breaking news

WENGER AWAONGEZEA MKATABA WAFARANSA WATATU

January 12th, 2017 | by mwana kabumbu
WENGER AWAONGEZEA MKATABA WAFARANSA WATATU
kimataifa
0

Arsene Wenger ametangaza habari njema kuwa wachezaji hao watatu muhimu wamesaini mkataba mpya huku Ozil na Sanchez wakisuasua

 Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin wamesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Arsenal, klabu hiyo imetangaza.

Wafaransa hao watatu wamekuwa watu muhimu katika kikosi cha Arsene Wenger misimu ya hivi karibuni, na Giroud akiwa kinara wa mabao wa klabu hiyo msimu uliopita na Koscielny akiwa mhimili mkuu wa beki nne.

“Tuna furaha kubwa kwamba wachezaji muhimu wa timu yetu wamesaini mkataba mpya wa muda mrefu,” alisema Wenger.

“Francis ameimarika sana kiufundi miaka kadhaa iliyopita kwa sababu anajituma kila siku.

“Olivier ana uzoefu mkubwa kwenye soka sasa na amekuwa zaidi na zaidi mchezaji kamili tangu alipojiunga nasi. Laurent ni mchezaji muhimu sana wa kikosi chetu na naamini ni miongoni mwa mabeki bora wa dunia leo hii. Kwa hiyo, kwa ujumla hizi ni habari njema kwetu.”

Habari hizi zimekuja kukiwa bado na utata juu ya mustakabali wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao wanahitaji mishahara mikubwa kufanya mkataba mpya na Washika Mtutu hao wa London.

SOURCE: GOAL.COM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *