breaking news

WAINGEREZA WAKATI NDIYO HUU AU BADO TUENDELEE KUSUBIRI KIZAZI KINGINE?.

March 29th, 2016 | by mwana kabumbu
WAINGEREZA WAKATI NDIYO HUU AU BADO TUENDELEE KUSUBIRI KIZAZI KINGINE?.
Fikra
0

FIKRA ZA MWANA KABUMBU:

Na: Aidan Mlimila

“Some people are on the pitch. They think it’s all over-It is now”. Ilikuwa ni mwaka 1966 kwenye Uwanja wa Wembley na hayo yalikuwa ni maneno ya mtangazaji wa shirika la Utangazaji la Taifa la Uingereza (BBC) wakati huo bwana Keneth Welstenholme.

Na hapo alikuwa akilitangaza goli la nne na la ushindi la Timu ya Taifa ya Uingereza (Three Lions) lililofungwa na mshambuliaji wa Uingereza Geoff Hurst. Ilikuwa ni mechi ya fainali ya kombe la dunia kati ya Timu ya Taifa ya Uingereza dhidi ya Timu ya Taifa ya Ujerumani (Iliyokuwa Ujerumani magharibi wakati huo). Uingereza walifanikiwa kushinda mechi hiyo kwa ushindi wa goli 4 dhidi ya 2 za Ujerumani. Na hivyo Uingereza wakafanikiwa kubeba ubingwa wa dunia kwa mara yao ya kwanza.

Tazama highlights za fainali za kombe la dunia 1966 hapa.

air-france-wreckage-pic-getty-image-3-218671548

Fainali za mwaka 1966 zilikumbwa na matukio kadhaa ya kukumbukwa katika historia ya kombe la dunia. Achana na goli la utata lilifungwa na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uingereza Geoff Hurst katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani magharibi goli ambalo lilipandikiza chuki kwa Wajerumani dhidi ya Waingereza, achana na kuibiwa kwa kombe (Jules Rimet Cup) ambalo baadae lilikuja kupatikana kwa msaada wa mbwa ambaye alijulikana kwa jina la pickles, achana na magoli tisa yaliyofungwa na mfungaji bora wa michuano hiyo mreno Eusebio.

[embedyt]https://www.youtube.com/watch?v=Fxx92BRf89w&width=640&height=400[/embedyt]

Tukio kubwa ambalo bila shaka linakumbwa sana na waingereza mpaka leo hii ni ile sauti ya mtangazaji wa shirika la Utangazaji (BBC) marehemu Kenneth Welstenholme  wakati akilitangaza goli la nne lililofungwa na Geoff Hurst ambalo liliwahakikishia waingereza  ubingwa. Unajua ni kwa nini hili tukio linakumbukwa sana? Jibu ni rahisi tu, ni kwa sababu ulikuwa ni ubingwa wao wa kwanza na wa mwisho kwa waingereza na kizuri zaidi ulikuwa ni ubingwa ambao walitwaa kwenye ardhi ya nyumbani tena mbele ya mashabiki wao.

Tangu Kenneth Welstenholme alitangaze goli lile la Geoff Hurst  mpaka sasa ni takribani miaka 50 imepita na waingereza hawajafanikiwa kutwaa kombe lingine lolote kubwa kwenye ngazi ya timu ya Taifa. Ni kipindi hiki hiki ambacho waingereza wameendelea kusubiri tumeshuhudia timu ya Taifa Ujerumani ambayo ilifungwa na timu ya taifa ya Uingereza mwaka huo 1966, ikichuchukua kombe la dunia mara tatu mwaka 1974, 1990, na 2014.

germany_champions1-640x360

Vimepita vizazi vingi ndani ya kipindi hiki cha miaka hiki cha miaka 50 ambayo waingereza wameendelea kusubiri pasipo kufanikiwa kutwaa kombe lolote lile kama ambavyo kina Bobby Moore na Sir Bobby Charlton walivyofanya mwaka 1966 pale Wembley na kumfanya Kenneth Wolstenholme asisimke wakati akilitangaza goli lile ambalo liliwahakikishia uingereza ubingwa.

Hapa katikati kuna kizazi ambacho waingereza walikiita kama kizazi cha dhahabu na kuamini kuwa kizazi kile cha dhahabu kingeweza kuyarudia ya yalifanywa na kina Geoff Hurst. Ni kizazi ambacho kiliundwa na nyota kadhaa kama Michael Owen,John Terry, Rio, Wayne Rooney, Ashley Cole, Frank Lampard, Steven Gerrard bila kumsahau David Beckham na wengine wengi. Kutokana na mseto huo wa nyota niliowataja hapo juu waingereza walikuwa na kila sababu ya kuamini kile ambacho walikuwa wanakiamini. Bila shaka ulikuwa  ni mkusanyiko wa Wachezaji ambao walistahili kuvaa medali yeyote ile wakiwa na timu ya Taifa ya Uingereza.

Wayne+Rooney+Frank+Lampard+England+v+Ukraine+URSoq4_JQ5bl

Kwa mshangao wa wengi kizazi hicho ambacho waingereza walikiona kama cha dhahabu akikufanikiwa kuvaa medali yeyote huku mafanikio yao makubwa yakiwa ni kufika hatua ya robo fainali.

Hivi karibuni tumeshuhudia timu ya Taifa ya Uingereza ikiifunga timu ya Taifa ya Ujerumani goli tatu kwa mbili katika mechi ya kirafiki iliyochezwa mjini Berlin, Ujerumani. Baada ya ile mechi kila mwingereza anaamini huu ndiyo wakati wao kuweza kufanya kitu kwenye fainali za Euro zitatazofanyika nchini Ufaransa.

kanevsgermany

Kwangu mimi kitendo cha Uingereza kuwafunga mabingwa wa dunia, Ujerumani siyo ishu kubwa sana kama ambavyo waingereza wengi wamefanya kuwa. Na hii inatokana na ukweli kwamba miaka yote waingereza wamekuwa ni mabingwa wa kucheza mechi za kirafiki na zile mechi za kufuzu. Lakini matatizo yao makubwa yamekuwa ni kuzicheza zile mechi za fainali zenyewe, ni kama ile laana ya wajerumani juu ya lile goli la utata la Geoff Hurst pale Wembley linaendelea kuwatafuna.

001E384E1000044C-3031532-image-a-4_1428565926082

 

Nikiitazama England ya sasa ambayo iko chini ya Roy Hodgson inaundwa na vijana wengi ambao hawana majina makubwa sana kama ambavyo kwenye kizazi kile kilichopita ambacho waingereza walikitambua kama kizazi cha dhahabu (Golden Generation). England ya sasa ya Hodgson inawategemea sana wachezaji wa Spurs kuliko Man utd ni mabadiliko, ndiyo ni mabadiliko. England ya sasa kwenye kiungo ina mtegemea Delle Ali na Eric Dier kutoka Steven Gerrard na Frank Lampard, ni mabadiliko ndiyo ni mabadiliko.

England ya sasa ina wachezaji wengi ambao ukiyatazama majina yao kwa mtazamo wa ukubwa wa majina na umaarufu bila shaka hayafiki walau nusu ya majina ya kile kizazi cha dhahabu kilichokuwa na wana mitindo wengi wakiongozwa na David Beckham.

687872-england-world-cup

Timu ya taifa ya Uingereza ya sasa ina wachezaji wengi ambao hawajaandikwa sana kwenye magazeti maarufu ya pale Uingereza kama ilivyokuwa kwa kizazi kile cha dhahabu. Nikiitazama Uingereza ya sasa nadhani wanaweza kufanya kitu  kwenye fainali za Euro pale Ufaransa. Moja kati ya sababu ambayo inanifanya nizidi kuamini kuwapa nafasi Uingereza ni aina ya vijana ambao wanaunda kikosi hicho cha simba watatu. Vijana wengi bado hawajathibitisha uwezo wao bila shaka watataka kuzitumia fainali hizi kufanya kile ambacho wazee wao wakiongozwa na Sir Bobby Charlton walikifanya mwaka 1966 na hivyo kuthibitisha uwezo wao.

England-national-team

 

 

Wachambuzi wengi wa masula ya soka wanazipa nafasi timu za Ujerumani, mwenyeji Ufaransa na bila kumsahau bingwa mtetezi Hispania na mimi bila kusita nawaongeza vijana wa Roy Hodgson katika kundi hilo la timu zinazopewa nafasi.

Kutoka kumtazama Wayne Rooney kama mtu ambaye waingereza walimtegemea kuweza kuwapa ubingwa mwaka 2010 pale Afrika ya Kusini mpaka sasa ambapo Jamie Vardy na Harry Kane wakitazamwa kama watu ambao wanaweza kurudia kile kilichofanywa mwaka 1966. Bila shaka kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa ligi kuu ya Uingereza hauwezi kujiuliza mara mbili juu ya uwezo wa Vardy na Kane katika kuzifumania nyavu. Na kizuri zaidi ni kwamba Vardy na Kane wako katika wakati ambao watataka kuthibitisha uwezo wao.

329C03FB00000578-0-image-a-28_1459161345937

Hakika miaka 50 ni mingi na ni vizazi vingi vimepita pasipo Uingereza kuvaa medali yeyote ile ya kimataifa, na ndiyo hapa ninapojiuliza swali hili “WAINGEREZA WAKATI NDIYO HUU AU BADO TUENDELEE KUSUBIRI KIZAZI KINGINE”? Jibu la swali hili tutalipata mara tu fainali za Euro zitakazofanyika pale Ufaransa kumalizika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *