breaking news

WACHEZAJI CHELSEA WAMJIA JUU DIEGO COSTA

January 16th, 2017 | by mwana kabumbu
WACHEZAJI CHELSEA WAMJIA JUU DIEGO COSTA
kimataifa
0

Weekend hii mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea Diego Costa aliachwa na kocha Conte kwenye mechi dhidi ya Leicester kutokana na kutokuwa na maelewano. Inasemekana kwamba Costa aligomea mazoezi ya viungo ya kocha huyo na kutupiana maneno mwisho wa siku kocha akaamua kumuacha kwenye kikosi hicho.Sababu nyingine inasemekana Costa anataka kwenda China ambapo ameahidiwa mshahara mkubwa.

Kutokana na taarifa mpya kutoka kwenye kikosi hicho ni kwamba wachezaji wa Chelsea wamemjia juu mchezaji huyo na kumtaka amalizane na kocha wao. Taarifa zaidi zinasema wachezaji hao wameona kwamba hali kama hii ndiyo ilisababisha kutofanya vizuri msimu uliopita.

Maelewano mabaya kati ya wachezaji na Jose Mourihno inasekana yalichangia sana perfomance mbaya ya kikosi hicho. Hivyo basi kutokana na mwenendo wao sasa hivi wakielekea kuchukua ubingwa hawataki kitu chochote kuharibu hali hiyo.

Baada ya Chelsea kucheza vizuri na kushinda mechi dhidi ya Leicester City, inaweza kuwa sababu ya kumfanya Costa awe mpole na kwenda kuyamaliza na kocha wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *