breaking news

TULIUSUBIRI USHINDANI HUU KWA MUDA MREFU KWENYE LIGI KUU TZ BARA

March 12th, 2016 | by mwana kabumbu
TULIUSUBIRI  USHINDANI HUU KWA MUDA MREFU KWENYE LIGI KUU TZ BARA
Fikra
0

 

TAFUKURI YA ANKO CHALAZA

Na Frank charles Gibebe

Ni  wazi kuwa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara imeonekana kuwa na mabadiliko makubwa uwanjani kwa baadhi ya timu zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu japokuwa changamoto za muda mrefu kama ubovu wa viwanja, uwezo wa baadhi ya timu kifedha pamoja na panga pangua ratiba ni vitu ambavyo vinaonekana kuwa kikwanzo kwenye ligi hiyo.

Nazungumzia suala la ushindani kwa sababu mpaka hivi sasa timu zikiwa zimecheza michezo 22,21 na 20 NI Ngumu kutabiri nani anaweza kuchukua ubingwa kutokana na ushinadani uliopo, ushindani huu unazihusisha Simba sc, Yanga sc Na Azam fc Timu hizi kila moja inaonekana kupambana kwa nguvu zote kwenye mechi  wanazocheza lengo ikiwa ni kuhakikisha kila mmoja anajitengenezea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Tafukuri ya Anko chalaza tunakufanyia uchambuzi kwa timu zote tatu ambazo zimeonekana kuchuana vikali kwenye mbio za ubingwa ,wadau wengi wa soka wengi wa soka wanaamini mechi mbili za mwisho ndio zinaweza kuamua bingwa hilo halina ubishi ila hili linaweza kutokea hasa kama shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Watakuwa makini na kudhibiti jambo lolote la upangaji wa matokeo ambalo linaweza kujitokeza kwenye mechi za Mwishoni.

SIMBA SC

simba

Mashabiki wengi wa Timu ya simba hawana furaha kwa muda mrefu ,ni ngumu kuwa na furaha kwa sababu timu yao wanayoipenda kwa dhati imeshindwa kutwaaa ubingwa wa ligi kuu ya vodacom {VPL}kwa misimu mitatu mfululizo,Mara ya mwisho simba kutwaa ubingwa ilikuwa ni msimu wa 2011/2012 kwa mashabiki na wapenzi wa simba ni vigumu kuridhika na hali hiyo

Hata hivyo ni kama furaha ya mashabiki hao inaanza kurejea taratibu chini ya kocha Jackson Mayanja ambaye tangu amerithi mikoba ya kukinoa kikosi hicho toka kwa kocha Raia wa uingereza Dylan Kerry timu hiyo imeonyesha mabadiliko kwenye ligi kuu ya vodacom kwa kufanya vizuri kwenye michezo yake japo kidonda cha uchungu kwa mashabiki kilitoneshwa na Yanga kwa kuifunga simba bao mbili bila majibu lakini wekundu hao wa msimbazi wamesahau yote kurejea kufanya vizuri kwenye ligi

simbadance

Simba sc ndio timu inayoongoza kwenye msimamo wa ligi kuu kwa kuwa na pointi 51 baada ya kucheza michezo 22 hivyo kuwa juu kwa mchezo mmoja dhidi ya watani wao timu ya Yanga na michezo miwili zaidi dhidi ya timu ya Azam fc kwa namna ambavyo simba imekuwa ikicheza uwanjani inaonyesha kuwa na mabadiliko kuanzia kwenye safu ya ulinzi,kiungo pamoja na ushambuliaji ambapo washambuliaji wake Ibrahim Hajib, Daniel Lyanga wameonekana kuwa na ushirikiano mzuri wakiongozwa na mshambuliaji machachari wa timu hiyo Hamis Kiiza ambaye mpaka hivi sasa ndio anaongoza kwa ufungaji akiwa na magoli 18.

Hii inaonyesha dhahiri tayari simba sc imeingia kwa kasi kwenye mbio za ubingwa na ni lazima Yanga na Azam watambue kuwa  hata kama wana mechi za viporo wasifikiri itakuwa kazi rahisi kumuondoa simba kwenye mbio za ubingwa, ukijaribu kuangalia mechi nyingi zilizobaki za simba zitachezwa hapa Dar es salaam kuliko za mkoani hivyo hii pia inaweza kuwa faida kwa timu hii.

YANGA SC

yanga (1)

Timu ya Yanga inafuatia ikiwa inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 Yanga ina faida ya mchezo mmoja kwani watani zao simba wao tayari wako juu zaidi kwa kucheza michezo 22 kuliko Yanga ambayo mpaka hivi sasa imeshacheza michezo 21

Wadau wengi wa soka wanaonekana kuipa nafasi timu hii ya kutwaa ubingwa hii ni kutokana na uwezo wa timu  ambao imekuwa ikiuonyesha tangu msimu uliopita na kuafanikiwa kutwaa ubingwa lakini msimu  huu makali yameongezeka zaidi baada ya kufanya usajili wa wachezaji kama Donard Ngoma Na Kamusoko ambao wanaonekana kuongeza nguvu na kasi ya Yanga Dimbani.

yanga-dance

Jambo ambalo linaweza kutia doa kwenye harakati za Yanga za kuwania ubingwa ni kutokana kuwa na ratiba ya mechi nyingi za mikoani kwenye ratiba yake ya mechi zilizobakia hii inaweza kuwa changamoto kwa Yanga kwa sababu viwanja vingi vya mikoani huwa ni vibovu sana lakini timu za mikoani kila moja itataka kufanya vizuri kwenye uwanja wake wa nyumbani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kubaki kwenye ligi kuu ya Vodacom  hili ni jambo ambalo benchi la ufundi la timu linapaswa kulizingatia na kuwa makini zaidi kwenye vita hii ya ubingwa kwa wababe watatu.

 

AZAM FC

azam(1)

Pengine ujio wa kasi wa klabu ya  Azam fc  umekuwa sababu ya yanayotukia leo kunako ligi kuu ya vodacom kwani kabla ya uwepo wa timu hii timu hizi mbili za simba na yanga zilikuwa zinapokezana ubingwa lakini tangu Azam imeingia kwenye lligi imetoa ushindani mkubwa sana ikiwa ni pamoja na kutishia utawala wa timu hizi kwenye soka la Tanzania.

Azam ni ya tatu kwenye msimamo ikiwa na ponti 47 ya michezo 20 hivyo na yenyewe bado inapewa nafasi ya kuchukua ubingwa, Tatizo la Azam fc msimu huu  ambalo linaweza kusababisha kuitoa kwenye mbio hizi ni kutokana na kuwa na Tabia ya homa ya vipindi kwenye mechi zake kwa sababu leo itafanya vizuri kesho kutwa utasikia imefanya vibaya hii inaweza kuwa tishio kwao kwenye mbio za ubingwa

azamdance

Ni lazima kocha Sterwat Hall kupambana kuhakikisha hali hii inapotea kwa kikosi chake ili kuendelea kutengeneza uwiano mzuri kwa timu hii kwenye mbio za ubingwa , Azam pia anakosa hamasa kubwa kama ilivyo kwa timu za simba na yanga kutokana na timu hizi kuwa na wingi wa mashabiki ambao wanaweza kuwa sehemu muhimu ya kukoleza raha ya timu hizi mbili mojawapo kuchukua ubingwa jambo ambalo kwa Azam fc halipo, mchezo wa simb sc dhidi ya Azam fc utakuwa na maana kubwa sana kwenye maamuzi ya ubingwa msimu huu.

Kwa ujumla bado kuna ushindani mkubwa sana kwa timu zote tatu lakini shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Wanapaswa kuwa karibu sana na waamuzi wanaochezesha kwenye mechi za ligi kuu ili kuhakikisha ladha hii ya ushindani haikatishwi na mkono wa mwenye nacho ili tuweze kushuhudia ushindani huu mpaka mwisho yawezekana kama umakini utakuwepo tunaweza kumsubiri bingwa wa ligi kuu ya vodacom kwenye michezo ya mwisho kabisa.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *