breaking news

TFF YAZINDUA MKAKATI KUELEKEA OLIMPIKI 2020 TOKYO

January 30th, 2017 | by mwana kabumbu
TFF YAZINDUA MKAKATI KUELEKEA OLIMPIKI 2020 TOKYO
Kitaifa
0
Shirikisho la soka nchini Tanzania limezindua mpango mkakati utakaoiwezesha Tanzania kupeleka timu ya mpira wa miguu kushiriki michuano ya Olimpiki 2020 inayotarajiwa kufanyika katika jiji la Tokyo nchini Japani.
Mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi wa michezo nchini,  Omar Yusuph, kwa niaba ya serikali alisema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na shirikisho la soka nchini katika kuhakikisha kuwa kuna maendeleo yanayofikiwa katika soka.
“Serikali inawapongeza sana, na inaahidi kuwaunga mkono katika kazi zenu, huku tukitanbua kuwa katika mchezo wowote bila ya kuanza na vijana hatuwezi kupata maendeleo” Alisema mkurugenzi huyo
Akizungumza awali wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es salaam leo, Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, alisema mpango huu unajumuisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 15, 17 na 19 ambao wanafuzu kucheza michuano hiyo.
“Tunashukuru kwamba tumefikia siku hii muhimu ambapo kama Watanzania wapenda soka tunajumuika kushudia kuanza safari ya pamoja kuelekjea kutimiza ndoto zetu” Alisema Malinzi
“Tumefanya juhudi kubwa na tunaomba kungwa mkono na wadau wote kwani ni gharama kubwa kuendesha mpira hasa soka la vijana, hata hivyo tumejizatiti ili kuhakikisha kuwa ndoto zetu zinafanikiwa” Aliongeza.
Naye mshauri wa soka la vijana nchini , Kim Polsen alisema kuwa mpira ni safari, na safari siyo hatima bali ni mwendo unao taka moyo wa kupambana, na aliipongeza TFF kwa kuanza safari hiyo kuelelekea Tokyo mwaka 2020
IMG_0008
Mshauri wa soka la vijana Kim Poulsen akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mpango mkakati kuelekea michuano ya Olimpiki 2020 Tokyo
“Nimefurahi kuhudhuria uzinduzi huu muhimu sana kwa hatima ya soka la Tanzania, nimefurahi pia kuwaona vijana wadogo ambo tumekuwa tukiwajenga kwa muda sasa ambao ninaamini watakuja kuwa wakombozi wa soka letu” Alisema Polsen
Wageni mbalimbali maarufu walikuwepo kwenye uzinduzi huo wakiwemo, Makamu wa Rais wa kamati ya Olimpiki Tanzania, Henry Tandau, mwenyekiti wa soka la vijana ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Dodoma, Mlamu Ng’ambi, kocha wa timu ya taifa Salum Mayanga na wengine wengi.
IMG_0034
Viongozi, wachezaji na wageni waalikwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi
wa kampeni kuelekea Tokyo 2020
IMG_0033
Mkurugenzi wa michezo Tanzania, Omari Yusuph akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa
kampeni  kuelekea Tokyo 2020
IMG_0028
Mkurugenzi wa michezo nchini , Omari Yusuph akitoa hotuba fupi katika ufunguzi wa
kampeni kuelekea Tokyo 2020
IMG_0019
Makamu wa Rais wa kamati ya Olimpiki Tanzania ,TOC, Henri Tandau, akitoa salaam
wakati wa uzinduzi kuelekea Tokyo 2020

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *