breaking news

SIMBA WAIKUNG’UTA MAJIMAJI GOLI 3

February 4th, 2017 | by mwana kabumbu
SIMBA WAIKUNG’UTA MAJIMAJI GOLI 3
Kitaifa
0

Klabu ya Simba leo wameiadabisha Majimaji ya Songea Bao 3-0  huku nyota ambao walikuwa hawapewi nafasi ya kuanza mara kwa mara katika kikosi hicho wakiongoza mauaji.

Mshambuliaji Ibrahim Ajib migomba ndie alikuwa sa kwanza kuzifumania nyavu za majimaji kabla ya kiungo Said hamis Ndemla kuweka msumari wa tatu na kupoteza matumaini ya majimaji.

Laudit Mavugo alishindilia msumari wa tatu na kuzidi kudidimiza ndoto za majimaji kubaki ligi kuu msimu huu.

Ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya wenyeji Majimaji ya Songea umeongeza maisha ya kocha Mcameroon Joseph Omog kuendelea kuhudumu ndani ya klabu ya Simba.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 48, ikiwa nyuma kwa pointi mmoja dhidi ya vinara Yanga wanaoongoza ligi kwa sasa wakiwa na pointi 49.

Katika mchezo wa leo washambuliaji Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu, walimaliza ukame wa mabao kwa kila mmoja kufunga bao na kujiongezea akaunti yake ya ufungaji msimu huu.

Hadi mapumziko Simba, Simba walikuwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Ajibu dakika ya 19, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Shiza Kichuya.

Majimaji walipambana kufa na kupona, kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo, lakini hawakuweza kumfunga kipa Daniel Agyei aliyefanya kazi kubwa ya kuokoa mashuti ya washambuliaji wa Majimaji.

Licha ya kuwa mbele kwa bao hilo lakini Simba walionekana kucheza kwa kujihami na kutumia mashambulizi ya kustukiza kwa kuwatumia Kichuya, na beki wake Mohamed Husseini ambao hata hivyo vijana wa Majimaji walionekana kujipanga vizuri na kuokoa hatari hizo.

Kipindi cha pili, Majimaji inayofundishwa na kocha Kally Ongala, ilikianza kwa kasi na kufanya shambulizi la hatari lakini mshambuliaji wake mkongwe Kelvin Sabato alishindwa kufunga akiwa amebaki na kipa Agyei.

Majimaji waliendelea kupambana kwa kuwachezea Simba nusu uwanja lakini katika harakati za kutafuta bao la kusawazisha walijikuta wakifungwa bao la pili dakika ya 63, mfungaji akiwa Said Ndemla aliyepiga shuti kali kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Mzamiru Yasini.

Pamoja na kufungwa, Majimaji waliendelea kuutawala mpira na kuwabana Simba huku wakifanya mashambulizi mengi lakini washambuliaji wake walionekana kukosa mbinu za kumalizia.

Laudit Mavugo alifunga bao la pili, baada ya kupokea pasi nzuri ya Jamvier Bukungu, na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Majimaji na kuamsha nderemo kwa kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo waliofika uwanjani hapo.

Ushindi huo unaifanya Majimaji kuzidi kuwa katika hali ngumu kwenye msimamo, na kuhitaji nguvu ya ziada ili kujinasua katika nafasi ya 14, iliyopo hivisasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *