breaking news

SEVILLA WAVUNJA MWIKO WA MADRID

January 16th, 2017 | by mwana kabumbu
SEVILLA WAVUNJA MWIKO WA MADRID
kimataifa
0

Real Madrid wameshidwa kufikisha michezo 40 bila kupoteza baada ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Stevan Jovetic kuchafua hali ya hewa dakika ya 90 goli ambalo limevuruga rekodi ya Madrid.

Ronaldo alianza kuiweka mbele Real Madrid dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati kufatia Dani Carvajal kufanyiwa faulo na golikipa wa Sevilla Sergio Rico.

Sergio Ramos akajifunga dakika ya 85 ukiwa ni mchezo ambao ulimkutanisha kwa mara nyingine na timu yake ya zamani.

Jovetic aliyeingia akitokea benchi, akafanya balaa kwa kmtungua golikipa wa Real Madrid Kaylor Navas na kuipa Sevilla ushindi.

Huo ni mchezo wa kwanza kwa Real kupoteza tangu April 6 huku wakiongoza msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi moja pekee mbele ya Sevilla iliyofikisha pointi 39 wakati Real inapointi 40.

Sevilla kwa sasa ipo nafasi ya pili kwa pointi moja juu ya Barcelona yenye pointi 38.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *