breaking news

SAMATTA AIKOA GENK APIGA GOLI DK 77

December 19th, 2016 | by mwana kabumbu
SAMATTA AIKOA GENK APIGA GOLI DK 77
kimataifa
0

Jana Jumapili December 18, Mbwana Samatta aliinusuru klabu yake ya KRC Genk kuchapwa kwenye uwanja wao wa nyumbani mbele ya Standard Liege mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji (Jupiler Pro League).

Samatta aliisawazishia Genk iliyokuwa nyuma kwa magoli 2-1 na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.

Genk walianza kupata goli la kuongoza dakika ya tatu (3) likifungwa na Omar Colley akimalizia assist ya Leon Bailey.

Dakika ya 15 Standard Liege walisawazisha bao kupitia kwa Sa, dakika 10 badae Standard wakapata bao la pili lililofungwa na Belfodil.

Akiwa ameanza katika kikosi cha kwanza, Mbwana Samatta akaokoa jahazi la Genk kwa kusawazisha goli kwa kichwa na kuifanya timu yake kuambulia pointi moja katika mchezo huo.

What a Coincidence! 

Mbwana Samatta anavalia jezi namba 77 halafu amefunga goli la kusawazisha dakika ya 77 zikiwa zimesalia dakika 13 mchezo kumalizika.

SOURCE: SHAFII DAUDA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *