breaking news

RONALDO MCHEZAJI BORA WA DUNIA

December 13th, 2016 | by mwana kabumbu
RONALDO MCHEZAJI BORA WA DUNIA
kimataifa
0
Unaweza kusema huu ni mwaka wa Cristiano Ronaldo hata kama unakwenda ukingoni.

Maana amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or . Ronaldo sasa anaichukua mara ya nne, akiwa alianza mwaka 2008 akiwa Manchester United na alipoingia Madrid, unaweza kusema hii ni ‘hat trick’.

Kabla haijawa Ballon d’Or, Ronaldo alichukua mwaka 2008, Messi akachukua mwaka 2009.

Baada ya kuwa Ballon d’Or, Messi amechukua mara nne miaka ya 2011, 2012, 2013 na 2015. Huku Ronaldo akiwa amechukua mara tatu katika miaka ya 2013, 2014 na 2016.

Kumbuka alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, akashinda Kombe la Euro akiwa na Ureno.

“Sikuwahi kufikiria kwenye maisha yangu kama ningeshinda tuzo hii mara nne. Nashukuru, najivunia na nimefurahi,” amesema Ronaldo.

“Ninawashukuru wachezaji wenzangu wote, timu ya taifa, Ral Madrid, watu wote na wachezaji nilioshirikiana nao kushinda tuzo hii binafsi.”

Hii hapa ni listi kamili ya wachezaji walioingia kwenye top 20 kuelekea kumtafuta mshindi wa Ballon Dor.

messi

[embedyt]https://www.youtube.com/watch?v=7XFanJxxew0&width=650&height=400[/embedyt]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *