breaking news

KOCHA MRENO AIKACHA AFRICAN LYON

January 19th, 2017 | by mwana kabumbu
KOCHA MRENO AIKACHA AFRICAN LYON
African Lyon
0

Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya African Lyon Bernado Tavares na msaidizi wake Joaquin Valinho juzi usiku wamesaini rasmi mkataba wa kuifundisha timu ya ligi kuu katika Visiwa vya Maldives ya New Radiant Sports Club.

Akizungumza na mtandao wa soka360 Bernado Tavares alisema “hii ni changamoto mpya kwangu na sababu hii timu huku ina mashabiki wengi sana na ni timu ambayo imekuwa ikishika nafasi za juu sana katika ligi ila kwa bahati mbaya msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya tano na sasa ni jukumu langu kuwarudisha kuwa namba moja tena”.

Lakini alidokeza kuhusu kufanya kazi Afrika “African Lyon wamenijenga kuhusu mazingira ya Afrika sina tatizo kurejea tena Afrika endapo ofa nzuri itakuja naipenda sana African Lyon lakini sina jinsi nina marafiki wrngi sana pale kuanzia wachezaji mpaka viongozi ile ni klabu yangu”.

Bernado Tavares na Joaquin Valinho walikaribishwa Maldives na tayari wameshasaini kandarasi ya kufundisha timu hiyo ya huko.

SOURCE: SOKA360

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *