breaking news

January 22nd, 2017 | by mwana kabumbu

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), wameanza vyema kulitetea taji lao kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ashanti United.

Mchezo  huo  uliochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku mlinda mlango Benno Kakolanya wa Yanga akiokoa mipira mingi ya hatari kwenye lango lake.

IMG-20170121-WA0038

Bao la kwanza la Yanga   lilifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Amis Tambwe  ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa Msuva.

Dakika 37  Yanga walipata bao la pili kupitia kwa Thaban Kamusoko  baada kuachia shuti kali nje ya kumi na nane lilomshinda mlinga mlango Rajabu Kahumbu.

IMG-20170121-WA0036

Msuva alifunga bao la tatu dakika ya 53 kwa penati baada ya Seleman Sultan kumchezea vibaya Msuva na muamuzi Ahmad Kikumbo kuamuru penati ipigwe na winga huyo akaweka mpira kambani.

Dakika 61  Ashanti wanapata goli la kufutia machozi lililofungwa na Isack Hassan ambaye aliwazidi ujanja mabeki wa Yanga.

IMG-20170121-WA0029

Yusuph Muhilu alikamilisha karamu ya magoli dakika ya 89 baada ya kufunga bao la nne kwa k umalizia krosi ya Emmanuel MartinYanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Amis Tambwe, Simon Msuva, Juma Mahadhi na kuwaingiza Matheo Anthoy, Emmanuel Martin na Yusuph Muhilu.

Kesho kutakuwa namchezo mwingine katika michuano hii katika ya Simba na Polisi Dar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

IMG-20170121-WA0032

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *