Ujerumani na Poland wamecheza kwa mara ya kwanza mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana baada ya mchezo wao wa Euro 2016 kumalizika huku kila timu ikiwa imeshindwa kupata bao katika kupambana kufuzu hatua ya mtoano.

Mario Gotze aliwahi kuambiwa na Joachim Low auonyeshe ulimwengu kuwa yeye ni bora kuliko Messi, na akafanya hivyo kwa kuifungia Ujerumani goli la ushindi Kombe la Dunia, lakini awamu hii mambo yanamwendea kinyuma.

Boateng na Hummels ambao wametoka kwenye hali ya majeruhi walionekana kucheza kizembe. Wakiwa wamefanikiwa kumficha Lewandowski, timu ambayo itakuwa kali kuliko Poland inaweza kuwashangaza Ujerumani kwa lundo la mabao. Carlo Ancelotti atakuwa amefuatilia kwa makini kuona jinsi mashine zake za ulinzi zinavyoendelea.

Timu zote sasa zina pointi 4 huku zikiwa zimebakiwa na mchezo mmoja ambao unaweza kuwahakikishia kufuzu kwa hatua inayofuata huku Ireland Kaskazini iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu ikitegemea matokeo mengine hata kama itashinda mchezo wake wa mwisho.

Mshambuliaji wa Poland Arkadiusz Milik alipoteza nafasi ya wazi kuifungia timu yake sekunde chache baada ya kuanza kipindi cha pili, mpira wa kichwa alioupiga akiwa hatua nne kutoka golini ukienda nje ya goli wakati kila mtu akiamini nyota huyo angepachika bao.

Wachezaji wawili wa Ujerumani Mario Gotze na Mesut Ozil walishindwa kufunga magoli baada ya Lukasz Fabianski kuchukua nafasi ya Wojciech Szczesny aliyeumia huku mashambuliaji wa Poland Milik akipoteza nafasi nyingine ya wazi kwenye usiku ambao angeiandikia historia nchi yake kwenye uwanja wa Stade de France.

Matokeo hayo yanaisukumiza Ukraine nje ya mashindano hayo kwasababu bado haina pointi hadi sasa.